Anayejilipua kwa kujitoa muhanga amekufa shahidi?

Swali: Ni ipi hukumu ya anayejilipua kwa kujitoa muhanga? Je, wanazingatiwa wamekufa wakiwa mashahidi?

Jibu: Mosi ili kujilipua kwa kujitoa muhanga kuzingatiwe ni kufa shahidi kwanza ni lazima kufanyike kwa ajili ya Allaah na sio ajili ya nchi. Pili ni lazima iwe chini ya uongozi wa Kiislamu unaoongozwa na mtawala muislamu.

Ama kuhusu mauaji haya yanayofanyika hii leo, basi itategemea kutokana na Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika kila kitendo kinategemea na nia na kila mmoja atalipwa kwa kile alichonuia. Yule ambaye kuhajiri kwake kutakuwa kwa ajili ya Allaah na Mtume wake, basi kuhajiri kwake kutakuwa kwa ajili ya Allaah na Mtume. Yule ambaye kuhajiri kwake kutakuwa kwa ajili ya dunia au mwanamke anayetaka kumuoa, basi kuhajiri kwake kutakuwa kwa lile aliloliendea.”

Kwa kufupiza ni kwamba haya malipuzi ya kujitoa muhanga sioni kuwa ni yenye kufaa isipokuwa chini ya uongozi wa Kiislamu. Kwa hivyo endapo tutakadiria kuwa mmoja katika watu hawa amefanya hivo kwa kutafuta uso wa Allaah, basi atalipwa kutokana na nia yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah wa Fataawaa al-Imaaraat (2)
  • Imechapishwa: 25/12/2020