Unapopitwa na swalah ya ´iyd

Imesuniwa kwa yule ambaye amepitwa na swalah ya ´iyd au amepitwa na sehemu yake kuilipa kwa sifa yake; aiswali Rak´ah mbili pamoja na Takbiyr zake zenye kuzidi. Kwa sababu ulipaji unasimulia utekelezaji. Pia kutokana na kuenea kwa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Kile mtakachokiwahi, kiswalini, na kile kilichokupiteni, kikamilisheni.”

Ukipitwa na Rak´ah pamoja na imamu basi ongezea nyingine.

Akija mtu akamkuta imamu anatoa Khutbah, basi atatakiwa kuketi chini kwa ajili ya kusikiliza Khutbah. Atakapomaliza basi ataiswali hali ya kuilipa.

Hapana neno kuilipa mtu kivyake au kwa mkusanyiko.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mulakhaswsw-ul-Fiqh (01/277)
  • Imechapishwa: 25/07/2020