Mfano wa matendo mema katika masiku kumi ya mwanzo ya Dhul-Hijjah

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna masiku ambayo matendo mema yanapendwa zaidi na Allaah ndani yake kama  masiku haya kumi.” Wakasema: “Hata Jihaad katika njia ya Allaah?” Akajibu: “Hata Jihaad katika njia ya Allaah. Isipokuwa mtu ambaye ametoka na nafsi yake na mali yake na asirudi na chochote katika hayo.”

Kuna aina mbalimbali ya matendo mema. Kwa mfano kusoma Qur-aan, kufanya Adhkaar, kusema ”Subhaan Allaah”, ”Alhamdulillaah”, ”Allaahu Akbar”, kuamrisha mema na kukataza maovu, kuswali, kutoa swadaqah, kuwatendea wema wazazi wawili na kuwaunga ndugu.

Ukitoa swadaqah ya pesa moja katika masiku kumi ya mwanzo ya Dhul-Hijjah na ukatoa swadaqah hiyhiyo katika kumi la mwisho la masiku ya Ramadhaan, ni kitendo kipi kinachopendeza zaidi kwa Allaah? Masiku haya kumi ya mwanzo ya Dhul-Hijjah. Swadaqah ndani yake inapendeza zaidi kwa Allaah kuliko swadaqah iliyotolewa kumi la mwisho la Ramadhaan.

Maswahabah wakasema: “Hata Jihaad katika njia ya Allaah?” Akajibu: “Hata Jihaad katika njia ya Allaah. Isipokuwa mtu ambaye ametoka na nafsi yake na mali yake na asirudi na chochote katika hayo.”

Kwa hiyo akajibu kwamba hata Jihaad katika njia ya Allaah ambapo Jihaad ndio nundu ya juu kabisa ya Uislamu. Isipokuwa tu katika sura moja peke yake:

”Isipokuwa mtu ambaye ametoka na nafsi yake na mali yake na asirudi na chochote katika hayo.”

Ametoka kwa nafsi yake na mali yake ambayo anapambana kwayo (kama mfano wa farasi au kipando kingine) ambapo akauliwa na asirejei na chochote, mnyama wake akauliwa na mali yake ikachukuliwa. Huyu ndiye  ambaye atakuwa mbora kuliko matendo mema katika masiku kumi ya mwanzo ya mwezi wa Dhul-Hijjah. Lisilokuwa hili matendo mema katika masiku haya yanapendeza zaidi kwa Allaah kuliko wakati wowote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binothaimeen.net/content/17549
  • Imechapishwa: 24/07/2020