Unapomsikia anayechemua na anayetoa salamu wakati wa Khutbah ya ijumaa

Swali: Kumtakia rehema anayechemua wakati wa Khutbah ya ijumaa?

Jibu: Asifanye hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ukimwambia rafiki yako siku ya ijumaa nyamaza ilihali huku imamu yuko anatoa Khutbah, basi umefanya upuuzi.”[1]

Kwa hivyo asifanye hivo na wala asiitikie salamu.

[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (716).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25209/هل-يجوز-تشميت-العاطس-اثناء-خطبة-الجمعة
  • Imechapishwa: 21/02/2025