Nimuombee du´aa mbaya anayekataa Sunnah kwa kiburi?

Swali: Anayekataa Sunnah kwa kufanya kiburi anaombewa du´aa mbaya?

Jibu: Aombewe uongofu. Pia akiombewa du´aa mbaya, basi mambo ni kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Basi kamwe hutoweza.”[1]

Kwa sababu alifanya kiburi.

[1] Salamah bin Akwa´ amesema:

“Mtu mmoja alikula kwa mkono wake wa kushoto mbele ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akasema: “Kula kwa mkono wako wa kulia.” Akasema: “Siwezi.” Ndipo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Basi kamwe hutoweza.” Hakuna kilichomzuia isipokuwa ni kiburi. Kisha baada ya hapo hakuweza tena kuupandisha kinywani mwake.” (Muslim (2021)).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25213/هل-يجوز-الدعاء-على-من-رفض-السنة-عنادا
  • Imechapishwa: 21/02/2025