Swali: Likisogezwa jeneza mbele ya imamu na mmoja wa waswaliji akajua kuwa maiti alikuwa haswali kabisa. Je, inafaa kwa mujibu wa Shari´ah kumweleza imamu?

Jibu: Udhahiri ni kwamba asimswalie ikiwa anatambua jambo hilo. Vinginevyo ushahidi wake mwenyewe pengine usikubaliwe. Lakini yeye akiacha kumswalia ndivo inavotakikana. Hapa ni pale anapojua kuwa alikuwa haswali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23623/حكم-من-علم-ان-صاحب-الجنازة-لم-يكن-يصلي
  • Imechapishwa: 01/03/2024