Baada ya ujenzi imebainika kuwa wamejenga msikiti juu ya kaburi

Swali: Kuna kijiji wamejenga msikiti na wakatumia pesa nyingi. Baada ya ujenzi kumalizika ikabainika kuwa wamejenga msikiti juu ya kaburi. Wanasema kuwa wakibomoa msikiti baada ya kutumia pesa nyingi itakuwa ni israfu.

Ibn Baaz: Hapana, wafukue kaburi. Hawakukusudia kujenga juu yake?

Muulizaji: Hapana.

Jibu: Walifukue kaburi kama ambavo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivoyafukua makaburi.

Swali: Hata kama msikiti umejengwa juu ya kaburi?

Jibu: Hata kama, kaburi lifukuliwe na litengwe mbali. Hawakukusudia kujenga juu ya makaburi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23622/ما-يفعل-من-بنوا-مسجدا-ثم-علموا-ان-تحته-قبر
  • Imechapishwa: 01/03/2024