Swali: Niligombana na mke wangu leo kuhusu kupika chakula cha shughuli na hakutekeleza agizo nililompa. Nikamwambia: “Wewe umetalikiwa, umetalikiwa, umetalikiwa.” Baadhi ya ndugu zangu walikuwepo na wakaniambia nitulie na nimtaje Allaah. Nikajutia nilichofanya. Nina watoto watatu naye na sasa hivi ana ujauzito. Naye ameridhia na mimi nimeridhia.
Jibu: Haya ni katika mambo ya kushangaza katika nyakati hizi. Unampa talaka kwa sababu tu hakukupikia chakula unavyotaka? Ikiwa amekosea kidogo katika kupika kwa mtazamo wako ndio umwache? Huyu ni mwanamke aliyekuzaalia watoto, ametoka kwa wazazi wake kwa heshima na thamani kubwa, halafu unamwacha kwa sababu ndogo kama hii? Hakika hili ni upungufu katika akili na upungufu katika dini. Haimpasi kabisa muumini kufanya jambo kama hili. Ama kuhusu hukumu ya talaka hiyo, suala hili linahitaji ufike mbele yetu binafsi ili tulitazame vizuri na kutoa fatwa kwa uhakika – kwa idhini ya Allaah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1306/من-طلق-زوجته-لخلاف-حول-الطعام
- Imechapishwa: 20/06/2026
Swali: Niligombana na mke wangu leo kuhusu kupika chakula cha shughuli na hakutekeleza agizo nililompa. Nikamwambia: “Wewe umetalikiwa, umetalikiwa, umetalikiwa.” Baadhi ya ndugu zangu walikuwepo na wakaniambia nitulie na nimtaje Allaah. Nikajutia nilichofanya. Nina watoto watatu naye na sasa hivi ana ujauzito. Naye ameridhia na mimi nimeridhia.
Jibu: Haya ni katika mambo ya kushangaza katika nyakati hizi. Unampa talaka kwa sababu tu hakukupikia chakula unavyotaka? Ikiwa amekosea kidogo katika kupika kwa mtazamo wako ndio umwache? Huyu ni mwanamke aliyekuzaalia watoto, ametoka kwa wazazi wake kwa heshima na thamani kubwa, halafu unamwacha kwa sababu ndogo kama hii? Hakika hili ni upungufu katika akili na upungufu katika dini. Haimpasi kabisa muumini kufanya jambo kama hili. Ama kuhusu hukumu ya talaka hiyo, suala hili linahitaji ufike mbele yetu binafsi ili tulitazame vizuri na kutoa fatwa kwa uhakika – kwa idhini ya Allaah.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1306/من-طلق-زوجته-لخلاف-حول-الطعام
Imechapishwa: 20/06/2026
https://firqatunnajia.com/unamtaliki-mama-watoto-wako-kwa-sababu-tu-hakukupikia-chakula/