Ibn Baaz kuhusu Hijaab nyeupe, kijani au nyekundu

Swali: Je, inajuzu kwa wanawake kuvaa nguo za rangi nyeupe?

Jibu: Inajuzu kuvaa nguo nyeupe ikiwa zimetengenezwa kwa mtindo sahihi ambao hauna kujifananisha na mavazi ya wanaume. Ikiwa kuna nakshi, ushonaji au umbo linaloifanya nguo hiyo kutofautiana wazi na ya wanaume, basi hakuna tatizo. Lakini kuvaa nyeupe kwa mtindo wa wanaume haijuzu, kwa sababu huko ni kujifananisha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani mwanamke anayejifananisha na mwanaume kwa mavazi. Hata hivyo ni sawa ikiwa mwanamke atavaa nyeupe, nyeusi au nyekundu, kwa mtindo usiojifananisha na wanaume. Wanaume pia huvaa nguo nyekundu, nyeusi, kijani na nyinginezo. Kilicho muhimu ni tofauti ya wazi kati ya mavazi ya mwanamke na ya mwanaume. Ikiwa mwanamke atajifananisha na mwanaume au mwanaume atajifananisha na mwanamke, basi wote wawili wamelaaniwa. Wanafaa wote wawili wajiepushe kabisa na kujifananisha. Mwanamke avae kilicho cha kwake na mwanaume avae kilicho cha kwake. Hili ndio jukumu kwa wote wawili.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1318/حكم-لبس-النساء-الثياب-البيض
  • Imechapishwa: 20/06/2026