Damu inayoendelea kumtoka mwenye nifasi baada ya siku 40

Swali: Ni ipi hukumu ikiwa mwanamke mwenye damu ya uzazi atasafika ndani ya siku arobaini kisha akaona damu baada ya arobaini au damu ikaendelea hadi siku khamsini?

Jibu: Anapofikisha siku arobaini na damu bado inaendelea, basi anatakiwa aoge. Kwa sababu mwisho wa nifasi ni siku arobaini kwa mujibu wa maoni sahihi. Ikiisha arobaini, basi anatakiwa aoge, aswali, afunge na anakuwa halali kwa mume wake. Ajihifadhi kwa pamba au mfano wake kutokana na damu hiyo. Damu hiyo baada ya hapo huwa ni damu ya kawaida, si damu ya uzazi. Ikikatika kisha ikarudi na ikakutana na kipindi cha ada yake ya hedhi anayoijua, basi anakaa kwa hedhi. Hiyo inakuwa ni hedhi, si damu ya uzazi. Ama damu hii inayoendelea kumtoka ni damu ya kawaida. Ajihifadhi kwa pamba na mfano wake, aoge, aswali, afunge na anakuwa halali kwa mume wake ndani ya damu hii iliyozidi arobaini. Kwa sababu muda wa damu ya uzazi ni siku arobaini, kama ilivyopokelewa katika Hadiyth ya Umm Salamah. Haya ndio maoni sahihi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1319/هل-الدم-بعد-الاربعين-من-النفاس
  • Imechapishwa: 20/06/2026