Swali: Mimi ni mtu mwenye msimamo. Lakini pamoja na hivyo ninahisi ususuwavu kwenye moyo wangu. Nifanye nini?

Jibu: Ee ndugu, usijisifu nafsi yako! Unasema kuwa una msimamo? Sema “nataraji kuwa nina msimamo – Allaah akitaka”. Allaah (Ta´ala) Amesema:

فَلَا تُزَكُّوا أَنفُسَكُمْ

“Basi msizitakase nafsi zenu.” (53:32)

Unajuaje kuwa una msimamo? Mtu mwenye msimamo alonyooka ni yule ambaye Dini, tabia na ´Aqiydah yake vimenyooka. Je, unajiamini kuwa na haya juu ya nafsi yako? Badala yake sema kuwa najitahidi kupambana na nafsi yangu kufanya ´amali.

Ama kuhusu ususuwavu kwenye moyo utibu kwa kumdhukuru sana Allaah, kusoma Qur-aan sana, kuhudhuria mizunguko ya darsa na elimu, swalah za usiku, kukaa na watu wema, jiweke mbali na chaneli na filamu na mikanda mibaya na michafu na marafiki wabaya. Kwa mambo haya imani yako itakuwa na nguvu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4716
  • Imechapishwa: 01/05/2015