Kinachozingatiwa ni maneno ya Allaah – na sio maneno ya watu

Swali: Kumeenea kupunguza ndevu kwa madai ya kwamba kuna tofauti kati ya wanachuoni. Ipi nasaha yako?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema katika Hadiyth Swahiyh:

“Punguzeni masharubu na zirefusheni ndevu, nendeni kinyume na majusi.”

Hadiyth zingine imekuja:

“Refusheni na fugeni.”

Haya ni maamrisho. Hoja ni katika Maneno ya Allaah na Mtume Wake. Kinachozingatiwa sio maneno ya watu. Maneno ya watu yanapimwa katika maneno ya Allaah na Mtume Wake. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ

“Mkizozana katika jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume.” (04:59)

Haya hapa Maneno ya Allaah na Mtume Wake.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ

“Enyi mlioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume.” (04:59)

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا

“Na kile anachokupeni Mtume basi kichukueni, na kile anachokukatazeni, basi kiacheni.” (59:07)

Haya hapa maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4716
  • Imechapishwa: 01/05/2015