Swali: Wanachuoni wametofautiana kuhusu maamuma kusoma al-Faatihah. Ni ipi kauli sahihi juu ya hilo?
Jibu: Wanachuoni wengi wanaonelea kuwa kisomo cha imamu katika swalah za kusoma kwa sauti kinatosheleza kwa maamuma. Wanachuoni wengine wakasema kuwa ni lazima kusoma al-Faatihah hata kwa maamuma. Wametumia dalili kwa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hana swalah yule ambaye hakusoma al-Faatihah.”
Wanachuoni wengi wametumia dalili Kauli Yake (Ta´ala):
وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ
“Inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na mkae kimya mpate kurehemewa.” (07:204)
Vilevile kwa Hadiyth:
“… na akisoma nyamazeni.”
Wakasema kuwa hii ni dalili kuonesha kuwa maamuma hasomi na anatakiwa kunyamaza. Kadhalika wana dalili zingine ikiwa ni pamoja na kwamba Muusa (´alayhis-Salaam) alikuwa akiomba na Haaruun akiitikia “Aamiyn”, ndipo Allaah Akasema:
قَالَ قَدْ أُجِيبَت دَّعْوَتُكُمَا
“Akasema: “Imekwishaitikiwa du’aa yenu.” (10:89)
Wanachuoni wengi wanaonelea hivi [kuwa maamuma anyamaze].
Baadhi ya wanachuoni wengine wanaonelea kuwa al-Faatihah ni yenye kufanyiwa Istithnaa´ katika Kauli Yake (Ta´ala):

“Inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na mkae kimya mpate kurehemewa.”
Hili ni kutokana na ujumla wa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

Vilevile kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Huenda mnasoma nyuma ya imamu wenu?” Wakasema: “Ndio.” Akasema: “Msifanye hivo isipokuwa tu kwa mama wa Qur-aan [al-Faatihah]. Kwani hana swalah yule asiyeisoma.”
Hii ndio kauli yenye nguvu kwangu. Ninaonelea kuwa kauli yenye nguvu kusoma al-Faatihah kumewekewa uvuliwaji. Isome pale ambapo imamu amekaa kimya. Hii ndio kauli sahihi na ndio ninayoitolea Fatwa.
- Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4716
- Imechapishwa: 01/05/2015

Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4716
Imechapishwa: 01/05/2015
https://firqatunnajia.com/ar-raajhiy-kuhusu-maamuma-kusoma-al-faatihah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)