ar-Raajhiy kuhusu ujinga ni udhuru 1

Swali: Ni ipi mizani kuhusiana na masuala ya kupewa udhuru kutokana na ujinga?

Jibu: Mjinga ambaye ana mtu wa kuuliza hapewi udhuru. Mjinga ni yule ambaye hajui masuala makubwa na yaliyojificha. Isitoshe vilevile ikawa mtu kama yeye anaweza kuwa hayajui na hana mtu wa kuuliza au hana hata kule kufikiria kuwa yana ubaya mpaka aweze kuyauliza. Ama mtu ambaye yuko na mtu wa kuuliza hapewi udhuru. Ni lazima kwake aulize. Allaah (Ta´ala) Amesema:

فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

“Basi ulizeni watu wenye ukumbusho ikiwa (nyinyi) hamjui.” (16:43)

Vilevile yule asiyetaki kuuliza hapewi udhuru. Kwa kuwa baadhi ya watu wanasema kuwa hawataki kuuliza ili jambo hilo lisimlazimu. Mtu kama huyu sio mwenye kupewa udhuru.

Anayepewa udhuru ni yule ambaye hana wa kumuuliza au kitu ambacho hakimjii hata kwenye fikira yake kama kinaweza kuwa na ubaya mpaka aweze kukiuliza. Ama kuhusu mjinga ambaye yuko na wa kuuliza au hataki hata kuuliza, huyu sio mwenye kupewa udhuru.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4716
  • Imechapishwa: 01/05/2015