´Umrah mara mbili kwa mwezi

801- Ahmad ametuhadithia: Humayd bin ´Abdir-Rahmaan ametuhadithia: Hammaam bin Yahyaa ametuhadithia:

“Qataadah aliulizwa kuhusu kufanya ´Umrah mara mbili kwa mwezi. Akasimulia kuwa Sa´iyd bin al-Musayyab, ´Atwaa´ na al-Hasan wamesema kuwa kitendo hicho hakina neno. Ibn ´Umar aliulizwa pia swali hilohilo na hakichukiza kitendo hicho.

802- Ahmad ametuhadithia: Yahyaa ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa az-Zubayr ambaye ameeleza kuwa amemsikia Jaabir aliulizwa juu ya ´Umrah baada ya masiku ya Tashriyq. Jawabu lake lilikuwa:

“Hakuna neno. Lakini hakutakiwi kuletwa mnyama wowote wa Udhhiyah.”

  • Mhusika: Imaam Abu Daawuud Sulaymaan bin al-Ash´ath as-Sijistaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 169-170
  • Imechapishwa: 26/03/2021