Usifarikiane na msikiti Mtakatifu namna hiyo

803- Ahmad ametuhadithia: Marwaan bin Mu´aawiyah al-Fazaariy ametuhadithia: ´Uthmaan bin al-Aswad ametuhadithia:

“Mujaahid alichukizwa mtu ambaye atasafiri kurudi kuanza kusimama katika mlango wa msikiti Mtakatifu, akaielekea Ka´bah, akaiangalia na kuomba du´aa. Amesema:

“Hivo ndivo mayahudi wanavofanya.”

804- Ahmad ametuhadithia: Marwaan bin Mu´aawiyah ametuhadithia: Rabaah bin Abiy Ma´ruuf ametuhadithia, kutoka kwa ´Atwaa´, kutoka kwa Ibn ´Abbaas ambaye amesema maneno mfano wa hayo.

  • Mhusika: Imaam Abu Daawuud Sulaymaan bin al-Ash´ath as-Sijistaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 170
  • Imechapishwa: 26/03/2021