826- Nimemsikia Ahmad akiulizwa kama inafaa kwa Muhrim kufunga kichwa chake kwa mkanda wa ngozi. Akajibu: “Hapana.” Kukasemwa: “Ikiwa ni kwa sababu kichwa kinamuuma?” Akajibu: “Hivyo basi atatoa kafara.”

827- Nilimuuliza Ahmad: “Je, Muhrim anaweza kufunika uso wake?” Akasema: “Ndio.” Nikauliza: “Je, anaweza kufunika nyusi zake?” Akajibu: “Ndio.” Nikauliza: “Je, anaweza kufunika masikio yake?” Akajibu: “Hapana.”

  • Mhusika: Imaam Abu Daawuud Sulaymaan bin al-Ash´ath as-Sijistaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 174
  • Imechapishwa: 26/03/2021