Umm Kulthuum bint Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

Alikuwa ni msichana wa nne kutoka katika nyumba ya kinabii.

Inasemekana kwamba aliolewa na ´Utaybah bin Abiy Lahab kisha baadaye akamwacha.

Aliingia katika Uislamu na akahajiri baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakati dada yake Ruqayyah alipofariki, akamuoza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa ´Uthmaan. Alikuwa bado ni bikira. Alimuoa katika Rabiy´ al-Awwal mwaka wa 03. Hata hiyo hakumzalia watoto.

Alifariki katika Sha´baan mwaka wa 09. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Lau ningelikuwa na wasichana kumi, basi ningeliwaoza kwa ´Uthmaan.”[1]

Anas bin Maalik ameeleza kwamba alimuona Umm Kulthum bint Rasuulillaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona akiwa na shuka ya juu ya iliochanganywa na hariri[2].

Anas bin Maalik amesema:

”Nilimuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akikaa karibu na kaburi lake na macho yake yanatokwa na machozi. Akasema: ”Katika yenu kuna yeyote ambaye hakufanya jimaa usiku?” Abu Twalhah akasema: ”Mimi.” Ndipo akasema: ”Shuka chini.” Ndipo akashuka chini kwenye kaburi.”[3]

[1] at-Twabaqaat al-Kubraa (8/38).

[2] al-Bukhaariy (10/252).

[3] al-Bukhaariy (3/126).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (2/252-253)
  • Imechapishwa: 05/10/2020