Swali: Je, ni katika Sunnah kusema:

كيف أصبحت

“Umeamkaje?”

Jibu: Hilo ni katika matendo ya waislamu. Hakuna chochote kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Maswahabah walimuuliza ´Aliy:

“Vipi hali ya Mtume? Mtume ameamkaje?”

Ameamka kwa himdi za Allaah hali ya kuwa amepona. Hayo ni maneno mazuri yanayotumiwa na waislamu. Yalisemwa na Maswahabah na waja wema.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24261/هل-قول-كيف-اصبحت-من-السنة
  • Imechapishwa: 20/09/2024