Swali: Maneno yake Ibn Mas´uud: “Baada ya kufishwa tukawa tunasema:

السلام على النبي

“Amani iwe juu ya Mtume.”?

Jibu: Hiyo ni Ijtihaad yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwafunza hivo. Aliwafunza waseme:

السلام عليك أيها النبي

“Amani iwe juu yako, ee Mtume.”

Hayo ndio mafunzo yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Sunnah ni kusema:

السلام عليك أيها النبي

“Amani iwe juu yako, ee Mtume.”

Kama alivowafunza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24258/هل-يصح-قول-السلام-على-النبي
  • Imechapishwa: 20/09/2024