Namna ya salamu kwa aliyeingia kwenye mkusanyiko wa watu wengi

Swali: Baadhi ya watu wanapoingia kwenye kikao wanatoa salamu na wanaketi chini na hawapeani mkono?

Jibu: Ni mwenye khiyari; akipeana mkono ni sawa, na akitoa salamu na akiketi chini ni sawa. Jambo ni lenye wasaa. Akipeana mkono kuonyesha kujali ni sawa. Na ikiwa kufanya hivo ni kuwatia watu uzito na akaona kuwa ni kuwatia watu uzito kwa sababu ni wengi, kule kukaa kwake chini pengine ndio kunawastarehesha watu ili asiwakalifishe. Hata hivyo akiwapa mkono asikemewe, kwa sababu Maswahabah walikuwa wanapeana mkono wanapokutana.

Swali: Sio jambo linalohimizwa kwa sababu ya kusamehewa madhambi?

Jibu: Wakati wa makutano kunapendeza. Maswahabah walikuwa wanapokutana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wanapeana mkono. Hata hivyo kikao cha watu kinaweza kuwa na mkusanyiko wa watu wengi na pengine jambo hilo likawachosha wao, yeye mwenyewe au akawashughulisha na ambayo ni muhimu zaidi. Kwa hiyo hali inatakiwa kuzingatiwa. Mwenye kuingia anatakiwa kuzingatia. Huenda wakachukulia vibaya kule kutowasalimia kwa kuwapa mkono wakaona kuwa amewadharau kama ambavo pengine wakaona kitendo hicho kinawaudhi na kuwatia uzito. Kwa hivyo mwenye kuingia anatakiwa kuzingatia mambo na asiwe mzembe.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24262/هل-الافضل-لمن-دخل-مجلسا-ان-يصافحهم
  • Imechapishwa: 20/09/2024