Swali: Maneno yake katika cheni ya wapokezi:

“Naapa kwamba Abu Dharr amenihadithia… “?

Jibu: Kwa kutilia mkazo. Ni kama mfano wa:

“Naapa kwa Allaah kule Allaah kumwongoza mtu mmoja kupitia kwako ni bora kwako kuliko ngamia wekundu.”[1]

Inafaa kwa msimuliaji, anayejibu maswali au mwanafunzi kuapa juu ya fatwa ikiwa yuko na uhakika wa hali ya juu. Lengo ni kutilia mkazo.

[1] al-Bukhaariy (3009) na Muslim (2406).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24263/حكم-الحلف-على-الفتوى-للتاكيد
  • Imechapishwa: 20/09/2024