Ujira kwa Allaah na kuondoshewa khofu na huzuni

Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالنَّصَارَىٰ وَالصَّابِئِينَ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ

“Hakika wale walioamini na wale ambao ni mayahudi na manaswara na masabai; yeyote yule ambaye atamwamini Allaah na siku ya Mwisho na akayafanya mema, basi watapata ujira wao kutoka kwa Mola wao na hakutokuwa na khofu juu yao na wala hawatohuzunika.”[1]

Hii ni hukumu inawahusu Ahl-ul-Kitaab peke yao. Kwa sababu maoni sahihi ni kwamba masabai ni miongoni mwa jumla ya makundi ya manaswara. Kwa hivyo Allaah akaeleza kwamba waumini kutoka katika Ummah huu, mayahudi, manaswara na masabai yule ambaye atamwamini Allaah katika wao na siku ya Mwisho na akawasadikisha Mitume yao, basi watakuwa na malipo makubwa na amani. Aidha hakutokuwa na khofu juu yao na wala hawatohuzunika. Kuhusu yule ambaye atamkufuru Allaah katika wao, Mitume Yake na siku ya mwisho basi atakuwa na hali kinyume na hii ambapo atakuwa  na khofu na huzuni.

Maoni sahihi ni kwamba hukumu hii kati ya mapote haya ni wao kama wao na si kwa nisba ya kumwamini Muhammad. Haya ni maelezo ya hali yao kabla ya kutumilizwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Baada ya Allaah kuwataja wana wa israaiyl na akawasema vibaya na pia akataja madhambi yao pengine jambo hilo likaingia ndani ya baadhi ya nafsi kwamba wote wanaingia katika kusemwa vibaya huko. Ndipo akataka (Ta´ala) kubainisha wale wasioingia katika wasifu huo wenye kusemwa vibaya. Aidha pale (Taa´ala) alipowataja  wana wa israaiyl peke yao ndipo akataja hukumu yenye kuenea inayohusu makundi yote ili haki ipate kuwa wazi, kuondoke kuelewa makosa na utatizi. Ametakasika Yule ambaye ameweka ndani ya Kitabu Chake yale yanayoshangaza akili za walimwengu!

[1] 02:62

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, uk. 45
  • Imechapishwa: 22/07/2020