Swali: Nini maana ya maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika miongoni mwa uzushi mkubwa mno ni mtu kusimulia kwa ambayo hakuona [usingizi].”?

Jibu: Maana yake ni kwamba miongoni mwa uwongo mkubwa ni mtu kuelezea ambacho hakuona. Kama vile kusema kuwa ameota kadhaa na kadhaa, akamsemea uwongo Allaah (Jalla wa ´Alaa) au akamsemea uwongo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni lazima kwa muumini kuchunga ukweli katika ndoto zake na maneno yake mengine yote.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23375/معنى-ان-من-اعظم-الفرى-في-الحديث
  • Imechapishwa: 05/01/2024