Swali: Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Asimweleze yeyote.”[1]

Ni kwa njia ya uharamu?

Jibu: Kuna upokezi mwingine unaosema:

“… isipokuwa anayempenda.”

Amweleze nayo anayempenda. Ndoto inayotokana na shaytwaan asimweleze yeyote.

Swali: Ni kwa njia ya machukizo au uharamu?

Jibu: Msingi ni kwamba makatazo yanapelekea katika uharamu. Huu ndio msingi. Hii ndio kanuni. Msingi wa makatazo yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yanapelekea katika uharamu. Isipokuwa yale yanayofahamisha kuwa inachukiza.

[1] Muslim (04/1772).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23374/ما-حكم-التحديث-بالروى-المنامية
  • Imechapishwa: 05/01/2024