Swali: Je, ni sahihi kwa mtu kusema juu ya mtu ambaye amegeuza usingizi wake mchana kwamba ameenda kinyume na Sunnah na maumbile?

Jibu: Hapana shaka kwamba ni kwenda kinyume na yale yaliyowekwa katika Shari´ah. Kilichowekwa katika Shari´ah ni kwamba akimaliza kuswali ´Ishaa alale. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amechukizwa na kulala kabla yake na kuongea baada yake. Kuna watu wengi hii leo wanakesha usiku na wanalala mchana. Huku ni kwenda kinyume na yale yaliyowekwa katika Shari´ah na kwenda kinyume na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23371/ما-حكم-من-يسهر-بالليل-وينام-بالنهار
  • Imechapishwa: 05/01/2024