Uhalisia wa mambo juu ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

Swali: Kuna baadhi ya watu wamenambia kuwa kuna Wahhaabiyyah ambapo mimi nikawaambia kuwa hakuna Wahhaabiyyah, ni madai yaliyozushwa na waovu ili kuwakimbiza watu na Da´wah yenye kutengeneza. Pamoja na hivyo kuna aliyenambia kuwa Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab alikuwa mwema [mwanzoni] lakini mwisho mwa uhai wake alipinda kwa sababu alipinga baadhi ya Hadiyth Swahiyh za Mtume kwa vile haziafikiani na maoni yake. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) ni katika walinganizi wakubwa wa Salafiyyah na ´Aqiydah iliosalimika na mfumo uliyonyooka. Vitabu vyake vinatolea ushahidi juu ya hayo.

Kuhusu uliyosema kuwa mpinzani wake mmoja amesema kuwa Shaykh mwishoni mwa uhai wake alipinda kwa vile alikataa baadhi ya Hadiyth Swahiyh kwa vile haziafikiani na matamanio yake, huu ni uongo na uzushi kwa Shaykh. Shaykh amekufa hali ya kuwa ni mtu mkubwa mwenye kuziheshimu Sunnah, kuzikubali, bali sivyo tu na kulingania kwazo (Rahimahu Allaah).

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/173-174)
  • Imechapishwa: 23/08/2020