Baadhi ya vitabu vyenye faida vya Tawhiyd na ´Aqiydah

Swali: Ni vipi vitabu vyenye kunufaisha katika kuifahamu ´Aqiydah?

Jibu: Vitabu vyenye faida katika kuifahamu ´Aqiydah vinatofautiana kutegemea na kutofautiana kwa watu katika kuvielewa, utamaduni na daraja zao za kielimu. Ni juu yake kumtaka ushauri mwanachuoni aliye karibu naye ambao wanajua hali yake, uwepesi wa kufahamu kwake na kujifunza elimu.

Miongoni mwa vitabu vyenye faida katika ´Aqiydah kwa njia ya kijumla ni pamoja na “al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah” na ufafanuzi wake, ufafanuzi wa “al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah”, “Kitaab-ut-Tawhiyd” cha Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab pamoja na ufafanuzi wake “Fath-ul-Majiyd” na ufafanuzi wake mwingine “Taysiyr-ul-´Aziyz al-Hamiyd”, “Kashf-ush-Shubuhaat” na “Thalaathat-ul-Usuwl” vyote viwili hivi ni vya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, “at-Tadmuriyyah” na “al-Hamawiyyah” vyote viwili hivi ni vya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, kitabu “at-Tawhiyd” cha Ibn Khuzaymah na Qaswiydah “an-Nuuniyyah” na ufafanuzi wake. Pamoja na kujua kuwa kitabu kikubwa na kitukufu kuliko vyote ni “Kitabu cha Allaah kikubwa”. Ndani yake mna ubainifu wa wazi kabisa juu ya ´Aqiydah sahihi na ubainifu wa yenye kuyabatilisha na kwenda kinyume nayo. Hivyo tunakuusia kukithirisha kukisoma na kuzingatia maana yake. Humo mna uongofu na nuru, uongofu juu ya kila kheri na matahadharisho juu ya kila shari. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ هَـٰذَا الْقُرْآنَ يَهْدِي لِلَّتِي هِيَ أَقْوَمُ

“Hakika hii Qur-aan inaongoza katika yaliyonyooka kabisa.” (17:09)

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/175-176)
  • Imechapishwa: 23/08/2020