Ufalme wote ni wa Allaah kwa hali yoyote ile

Lau viumbe wote, kuanzia wa mwanzo wao mpaka wa mwisho wao, majini na watu, wote watakuwa wachaji Allaah kwenye moyo wa mtu mmoja, hilo halizidishi chochote katika ufalme wa Allaah. Ufalme ni wa Kwake Yeye. Ufalme sio wa wema wala wa waasi. Vilevile lau viumbe wote, kuanzia majini na watu, wa mwanzo wao mpaka wa mwisho wao, wote watakuwa wanatenda maasi na wakawa kwenye moyo wa mtu mmoja muovu, hilo halipunguzi chochote katika ufalme wa Allaah. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنكُمْ ۖ وَلَا يَرْضَىٰ لِعِبَادِهِ الْكُفْرَ ۖ وَإِن تَشْكُرُوا يَرْضَهُ لَكُمْ

“Mkikufuru, basi hakika Allaah ni mkwasi kwenu, na wala haridhii kwa waja Wake ukafiri na mkishukuru huridhika nanyi.” (39:07)

Ufalme wa Allaah (´Azza wa Jall) haupungui kwa maasi ya watenda maasi kama ambavyo hauzidi kwa ´ibaadah za watenda mema. Ni ufalme wa Allaah kwa hali yoyote ile.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/136)
  • Imechapishwa: 04/03/2024