Msisitizo wa kuzidisha matendo mema mwishoni wa umri

Linalotakikana kwa mtu kila ambavyo umri wake unazidi kuwa mrefu ndivyo azidishe kutenda matendo mema. Vilevile hata kwa kijana inatakikana azidishe matendo mema. Mtu hajui ni lini atakufa. Anaweza kufa katika ujana wake na kufa kwake kunaweza kuchelewa. Lakini ni jambo lisilokuwa na shaka juu ya kwamba yule ambaye umri wake umezidi kusogea mbele zaidi yuko karibu na mauti zaidi kuliko kijana kwa sababu umri wake unazidi kuyoyoma.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/139)
  • Imechapishwa: 04/03/2024