Swali 50: Mwanafunzi atamnasihi vipi mwalimu wake?

Jibu: Kinachotakikana ni kinyume chake kwamba mwalimu ndiye ambaye anamshauri mwanafunzi. Kwa sababu mwalimu ndiye anayekuwa mjuzi zaidi na mtambuzi zaidi wa mambo. Mwalimu bado ni mwenye kuendelea kujifunza elimu kutoka kwa mwalimu wake. Pengine mwanafunzi ikamdhihirikia jambo ambalo anafikiri kuwa ni kosa lakini ukweli wa mambo si kosa.

Pindi mwanafunzi anapotatizika na jambo basi analazimika kumuuliza mwalimu wake kwa adabu[1].

Lakini ikiwa mwalimu ni mpotofu au anayeenda kinyume, basi haijuzu kusoma kwake.

Ama ikiwa mwalimu analazimiana na haki lakini akateleza, basi unapaswa kumshauri kwa njia ya swali. Kwa mfano muulize hukumu ya anayefanya kitendo fulani. Atazinduka na kutafikiwa malengo – Allaah akitaka.

[1] Salaf walikuwa wakiwatukuza na kuwathamini waalimu zao, wakizitambua haki zao na wakifanya nao adabu. Hili ndio jambo la wajibu. ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Miongoni mwa haki za mwanachuoni juu yako unapofika kwake msalimie yeye khaswa na wengine kwa jumla, uketi mbele yake, usimuashirie kwa mkono wako na usikonyeze kwa macho yako. Usiseme kuna mwingine anayesema kinyume na maoni yako. Usishike nguo zake. Using´ang´anie pindi unapomuuliza maswali. Yeye ni kama mtende uliobeba tende tosa; bado kitu katika tende hizo zinaendelea kukuangukia.” (Jaamiy´ Bayaan-il-´Ilm wa Fadhwlih, uk. 231)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 137
  • Imechapishwa: 04/03/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy