Ufafanuzi kuhusu kuchukua kodi kutoka kwa wasio watu wa Kitabu

Swali: Waislamu wanapoingia katika nchi ya ukafiri kwa ajili ya kuifungua, je, imesuniwa kwao kuchukua kodi na kutowapiga vita au kodi huchukuliwa kwa watu wa Kitabu tu?

Jibu: Ikiwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amerahisisha hilo na amri ya jihaad imesimama na waislamu wakaingia katika nchi za ukafiri, basi wao ni makundi. Kama ni mayahudi, manaswara au waabudia moto na watakubaliwa kulipa kodi na hawapigwi vita wanapolipa kodi. Nayo ni mali inayochukuliwa kutoka kwao kila mwaka kulingana na hali zao na huwekewa na mtawala wa waislamu kwa manufaa ya waislamu, kwa kuwasaidia waislamu, kwa kuwadhilisha wao na kwa njia hiyo huenda wakanyenyekea na kuingia katika dini ya Kiislamu baada ya hapo. Ama kama ni waabudu masanamu – si mayahudi, manaswara wala waabudia moto, bali ni makundi mengine – basi lililo mashuhuri kwa wanazuoni ni kwamba wanapigwa vita; ama kuingia ndani ya Uislamu au vita na wala hawakubaliwi kulipa kodi. Jopo la wanazuoni wengine wamesema kwamba hakuna tatizo kuchukua kodi kutoka kwa makafiri wote, isipokuwa tu waarabu, kwa kuwa waarabu hawakukubaliwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwakubali, bali aliwapiga vita mpaka wakaingia katika dini ya Allaah. Ama wasiokuwa waarabu miongoni mwa watu wote wasio waarabu, basi wameona kuwa hakuna tatizo wakakubaliwa kulipa kodi wakiitoa hata kama si mayahudi, manaswara wala waabudia moto, bali ni watu wa dini nyingine na dini nyingine za kuabudu masanamu na na nyenginezo. Hawa wanakubaliwa kulipa kodi kwa mtazamo wa wanazuoni wengi. Mtawala wa waislamu anaangalia hilo. Baada ya Ufunguzi anaangalia manufaa; akiona manufaa ya Kishari´ah ni kuwakubalia kulipa kodi, basi anawakubali, na akiona manufaa ya Kishari´ah ni kuwapiga vita mpaka waingie Uislamu, basi anawapiga vita, kama walivyosema wanazuoni wengi. Kuhusu mayahudi, manaswara na waabudia moto hawa wanazuoni wameafikiana kwa maafikiano kwamba kodi hukubaliwa kutoka kwao kwa maandiko ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa maandiko ya Qur-aan kuhusu mayahudi na manaswara. Basi wakitoa kodi mayahudi, manaswara na waabudia moto, basi inawajibika kuichukua kutoka kwao, kuwakubalia juu ya dini yao na kuwalinda dhidi ya maadui zao mpaka waingie Uislamu au waendelee kulipa kodi wakiwa wanyenyekevu kwa masharti yaliyowekwa juu yao na wakiyatekeleza.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2211/حكم-اخذ-الجزية-من-الكفار-غير-اهل-الكتاب
  • Imechapishwa: 18/07/2026