Swali: Nje ya nchi yetu wanaishi pamoja na familia za manaswara kwa kisingizio kwamba wanajifunza lugha kutoka kwao. Lakini wakati huohuo wanakunywa pombe pamoja nao, wanakula nyama ya nguruwe pamoja nao, wanaacha swalah na swawm kwa kujipendekeza na kujikombakomba kwao na mengineyo katika kuichafua sura ya dini na watu wake. Kisha hurudi wakiwa ni maadui wa Uislamu na waislamu. Ni yepi maoni ya serikali yetu yenye uongozi mwema katika jambo hili?
Jibu: Hili limeshatanguliwa kulizungumza. Hili ni miongoni mwa yale yaliyotanguliwa kuyataja na kwamba hili halijuzu na wala haitakiwi kuwatuma kabisa. Wakishatumwa kisha wakaruhusiwa kushuka na kukaa katikati ya makafiri na ndani ya nyumba zao, basi jambo linakuwa khatari zaidi. Hili bila shaka limekatazwa. Lengo ni kuwapeleka wanafunzi kusoma nje ya nchi, lakini lililo wajibu ni kujali utekelezaji na kufuatilia utekelezaji. Wale wanaoamrishwa kuishi miongoni mwa familia kwa kisingizio cha kujifunza lugha na iwe rahisi kwao kuelewa lugha kwa mfano ya Kiingereza, hili ni katika hila za shaytwaan na katika misukumo ya shaytwaan, kwani huwachochea kati yao na familia zao. Hili liko karibu zaidi na uovu na kubwa zaidi katika khatari ya kwenda katika uzinifu, kunywa pombe, uharibifu wa ´Aqiydah, uharibifu wa maadili na mengineyo. Lau wangekuwa mbali kwa vipimo vya lugha, mbali na familia na mbali na wanawake, basi ingekuwa salama zaidi. Kwa hiyo kushuka kwa mwanafunzi miongoni mwa familia za makafiri, ndani ya nyumba zao na kulala kwao, hili bila shaka ni jambo ovu kubwa na khatari. Haijuzu kubaki kabisa. Nchi inapaswa kulizuia jambo hili kikamilifu. Aidha ni juu yetu na juu ya wanazuoni wengine kujitahidi katika jambo hili na kuwanasihi watawala ili lisionekane tena na ili waislamu waokoke na shari ya wazo hili batili na mambo haya batili.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2186/حكم-السكن-مع-العاىلات-النصرانية-بحجة-اكتساب-اللغة-الانجليزية
- Imechapishwa: 18/07/2026
Swali: Nje ya nchi yetu wanaishi pamoja na familia za manaswara kwa kisingizio kwamba wanajifunza lugha kutoka kwao. Lakini wakati huohuo wanakunywa pombe pamoja nao, wanakula nyama ya nguruwe pamoja nao, wanaacha swalah na swawm kwa kujipendekeza na kujikombakomba kwao na mengineyo katika kuichafua sura ya dini na watu wake. Kisha hurudi wakiwa ni maadui wa Uislamu na waislamu. Ni yepi maoni ya serikali yetu yenye uongozi mwema katika jambo hili?
Jibu: Hili limeshatanguliwa kulizungumza. Hili ni miongoni mwa yale yaliyotanguliwa kuyataja na kwamba hili halijuzu na wala haitakiwi kuwatuma kabisa. Wakishatumwa kisha wakaruhusiwa kushuka na kukaa katikati ya makafiri na ndani ya nyumba zao, basi jambo linakuwa khatari zaidi. Hili bila shaka limekatazwa. Lengo ni kuwapeleka wanafunzi kusoma nje ya nchi, lakini lililo wajibu ni kujali utekelezaji na kufuatilia utekelezaji. Wale wanaoamrishwa kuishi miongoni mwa familia kwa kisingizio cha kujifunza lugha na iwe rahisi kwao kuelewa lugha kwa mfano ya Kiingereza, hili ni katika hila za shaytwaan na katika misukumo ya shaytwaan, kwani huwachochea kati yao na familia zao. Hili liko karibu zaidi na uovu na kubwa zaidi katika khatari ya kwenda katika uzinifu, kunywa pombe, uharibifu wa ´Aqiydah, uharibifu wa maadili na mengineyo. Lau wangekuwa mbali kwa vipimo vya lugha, mbali na familia na mbali na wanawake, basi ingekuwa salama zaidi. Kwa hiyo kushuka kwa mwanafunzi miongoni mwa familia za makafiri, ndani ya nyumba zao na kulala kwao, hili bila shaka ni jambo ovu kubwa na khatari. Haijuzu kubaki kabisa. Nchi inapaswa kulizuia jambo hili kikamilifu. Aidha ni juu yetu na juu ya wanazuoni wengine kujitahidi katika jambo hili na kuwanasihi watawala ili lisionekane tena na ili waislamu waokoke na shari ya wazo hili batili na mambo haya batili.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2186/حكم-السكن-مع-العاىلات-النصرانية-بحجة-اكتساب-اللغة-الانجليزية
Imechapishwa: 18/07/2026
https://firqatunnajia.com/khatari-ya-wale-waislamu-wanaotumwa-katika-nchi-za-makafiri-kwa-ajili-ya-kujifunza-elimu-zao/