Udhhiyah kwa aliyekusudia kuhiji

Swali: Ni ipi hukumu ya kuchinja Udhhiyah kwa aliyekusudia kuhiji? Je, amnunue katika nchi yake na kumgawanya au ni sawa pia endapo atamnunua Makkah na kumchinja huko?

Jibu: Jambo ni lenye wasaa. Lakini kama yuko na familia basi bora amchinje nchini mwake kwa ajili ya watoto na watu wa nyumbani kwake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (15)
  • Imechapishwa: 03/07/2020