Twawaaf-ul-Ifaadhwah haina wakati wa mwisho

Swali: Je, ni sahihi kuchelewesha Twawaaf-ul-Ifaadhwah mpaka Muharram?

Jibu: Ndio, ni sahihi. Twawaaf-ul-Ifaadhwah inaanza baada ya nusu ya usiku wa tarehe 10 na haina mwisho wake. Wakati atapofanya Twawaaf hiyo itasihi kwake, lakini kwa sharti asimwingilie mke wake mpaka kwanza afanye Twawaaf-ul-Ifaadhwah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (23) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-13-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 03/07/2020