Swali: Je, Anaashiyd na maigizo ni miongoni mwa mambo yaliyozuliwa na watu kwa jili ya kuwavuta vijana?

Jibu: Anaashiyd na maigizo ni Bid´ah. Kuhusu Anaashiyd ni miongoni mwa nyimbo za Suufiyyah. Walizizusha kwa ajili ya kulainisha nyoyo kwa madai yao. Kisha baada ya hapo shaytwaan akawaghuri na wakawa wanataka ziimbwe na mtu ambaye yuko na sauti nzuri. Halafu baada ya hapo wakaona kuwa mwimbaji mmoja hatoshi; ni lazima kuwepo kikosi cha watu wanaozirudiarudia kwa pamoja. Mara nyingi watu hawa wanakuwa ni vijana wenye sauti nzuri na wenye muonekana mzuri. Namna hivi ndivo zilivyoendelea hatua kwa hatua.

Ama kuhusu maigizo, tunatambua kuwa Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walipigana vita kila mahali na wakawalingania katika Uislamu na hawakuhitajia maigizo haya. Bali ukweli wa mambo ni kwamba maigizo haya huenda yakaita katika maovu.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fath-ur-Rahiym al-Waduud, uk. 256-257
  • Imechapishwa: 03/07/2020