Ubora wa kudumua na mema na wakati fulani mtu akazuilika

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mja anapogonjweka au akasafiri, basi anaandikiwa mfano wa aliyokuwa akiyafanya wakati ambapo ni mkazi na mzima.”

Yule mwenye kutamani kheri na kuipupia, ikiwa katika ada yake anaifanya kheri hiyo lakini akafikwa na udhuru miongoni mwa nyudhuru, basi anaandikiwa ujira kikamilifu. Kwa mfano mtu ana ada ya kuswali pamoja na mkusanyiko msikitini lakini akawa amefikwa na udhuru, kwa mfano kupitikiwa na usingizi, ugonjwa na mfano wa hayo, basi anaandikiwa ujira kama wa aliyeswali pamoja na mkusanyiko. Anaandikiwa kikamilifu bila ya upungufu. Vivyo hivyo ni katika ada yake kuswali swalah za sunnah lakini hata hivyo akafikwa na kizuizi na akawa hakuweza kuiswali, anaandikiwa ujira kikamilifu. Vilevile ikiwa ni katika ada yake kufunga siku tatu kila mwezi kisha akafikwa na kizuizi na akashindwa kufanya hivo, anaandikiwa ujira kikamilifu. Mifano kama hiyo ni mingi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/36)
  • Imechapishwa: 18/01/2023