Baada ya kumpa zakaah masikini imebainika kuwa ni tajiri

Mtu akitoa zakaah kumpa mtu ambaye anafikiri kuwa ni miongoni mwa wale wanaostahiki kupewa zakaah na baadaye ikaja kubainika kuwa ni tajiri na sio miongoni mwa wanaostahiki kupewa zakaah, basi zakaah yake inatosheleza na ni yenye kukubalika na dhimmah yake imesafika. Kwa sababu alinuia kumpa yule ambaye inamstahikia. Akinuia ana nia yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/40)
  • Imechapishwa: 18/01/2023