Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

61 – Hakuna ambaye mguu wake utakuwa imara katika Uislamu isipokuwa kwa kujisalimisha.

MAELEZO

Uislamu sahihi hausimami isipokuwa kwa kujisalimisha kwa Allaah (´Azza wa Jall). Amesema (Subhaanah):

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

“Naapa kwa Mola wako! Hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu katika yale wanayozozana kati yao kisha wasipate katika nyoyo zao uzito katika yale uliyohukumu na wajisalimishe kwa kujisalimisha.”[1]

Kujisalimisha maana yake ni kunyenyekea na kutii yale yote yaliyokuja kutoka kwa Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] 4:65

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 82
  • Imechapishwa: 18/01/2023