Uashiriaji kidole katika Tashahhud kwa ambaye kimekatika kidole chake

Swali: Vipi ikiwa kidole cha kuashiria kimekatika?

Jibu: Udhahiri – na Allaah ndiye Mjuzi zaidi – ni kwamba akiashiria kidole cha kati au kidole gumba, yote ni kheri – Allaah akitaka. Lengo ni kufanya ishara ya upwekeshaji. Inatosha akiashiria kwa kutumia vidole alivyonavyo. Kama kuna kitu alichobaki nacho na akaashiria nacho inatosha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24858/حكم-الاشارة-في-التشهد-لمن-سبابته-مقطوعة
  • Imechapishwa: 20/12/2024