Twahara haichenguki kwa kumalizika muda wa soksi au kuzivua

Elewa ya kwamba twahara ya mtu haichenguki kwa kumalizika muda wa kupangusa juu ya soksi. Lakini endapo wudhuu’ wake utachenguka, ni lazima avue soksi zake na kuosha miguu. Lakini hata hivyo kule muda kuisha hakuchengui wudhuu’.

Vilevile akizivua baada ya kupangusa juu yake, wudhuu’ wake hauchenguki. Anabaki na wudhuu’ wake. Atapotaka kutawadha tena ni lazima aoshe miguu yake baada ya kuwa ameshazivua. Kanuni ya hili, ili mambo yasikanganye, ni kwamba: pale kinapovuliwa kilichopanguswa juu yake hakirudi kupanguswa tena. Ni lazima aoshe mguu kisha ndio anaweza kupangusa tena ikiwa anataka kutawadha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/373)
  • Imechapishwa: 17/05/2023