Tuzae au tusizae – haki ni ya mwanamke

Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kuangusha haki yake ya kuzaa, pasi na kujali sababu inatokana na kasoro kwa mume au yeye ndiye anayependa kuendelea kuishi naye kwa sababu yeye mume hataki kuzaa watoto?

Jibu: Mwanamke akiridhia jambo hilo ya kwamba mume hazai, inafaa kwake kufanya hivo. Haki ni yake yeye mwanamke.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (37)
  • Imechapishwa: 21/07/2023