Swali: Wanasema tukiacha kupiga kura, tunawaachia nafasi wengine…

Jibu: Waache. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Baki nyumbani kwako.”[1]

”Vinginevyo bora yakufike mauti na huku ukiuma shina la mti.”[2]

Uko wapi wasia wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati mambo ya watu yameparanganyika na yamekuwa vurugu?

Anayesema hivo ndiye ambaye moyo wake una maradhi na matamanio. Hakuna jengne anachotaka isipokuwa cheo. Watu kama hawa, kwa mujibu wa Shari´ah, huwa hawapati nafasi yoyote. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Naapa kwa Allaah! Kazi hii hatumpi yule mwenye kuiiomba.”[3]

Ambaye anazungumza namna hiyo anafanya hivo kwa sababu ya kupenda shari na sio kwa sababu ya kuipenda Shari´ah. Hata kama utashiriki, hutopata nafasi yoyote baadaye. Baada ya hapo itajengwa serikali au nafasi zitagawanywa. Nafasi fulani inachukua mwanamke, nafasi nyingine inachukua mwanasekula mwanamke fulani, nafasi nyingine inachukua mtu ambaye haswali kabisa na kadhalika. Je, kuna lolote unaweza kusema baada ya kuwa watu hawa wameshakaa nafasi zao? Kamwe. Kwa hivyo ufumbuzi ni kuwaepuka watu hawa na kusubiri mpaka pale Allaah atawapa waislamu mtawala mwema. Kujengea hoja kwamba tusiwaachie nafasi watu hawa… hata kama ukishiriki hutofaulu. Haiwezekani.

[1] Abu Daawuud (4263).

[2] Abu Daawuud (1708).

[3] Muslim (1733).

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Aliy bin Aadam al-Ithyuubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?app=desktop&v=V16FubR1VWQ
  • Imechapishwa: 07/09/2022