Swali 60: Akisahau ambaye amejiunga na imamu baada ya kupitwa na sehemu ya swalah imesuniwa kwake Sujuud ya kusahau? Ni lini atasujudu? Je, maamuma wanalazimika kuleta Sujudu ya kusahau wanaposahau?

Jibu: Maamuma hawana Sujuud ya kusahau wanaposahau. Ni lazima kwao kumfuata imamu wao wakiwa wamejiunga naye kuanzia mwanzoni mwa swalah. Kuhusu ambaye amekuja baada ya kuchelewa sehemu ya swalah yeye atatakiwa kusujudu Sujuud ya kusahau akisahau nyuma ya imamu wake au kwa yule ambaye anaswali peke yake baada ya kumaliza swalah pamoja na imamu kwa mujibu wa upambanuzi uliotangulia katika majibu ya maswali mawili yaliyotangulia 58, 59.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 64
  • Imechapishwa: 07/09/2022