Ruwaym alipewa mtihani na Ghulaam Khaliyl ambaye amesema juu yake:

“Mimi nimemsikia akisema: “Hakuna kati yangu mimi na Allaah pazia.”

Baada ya hapo akakimbia Dameski na akajificha kwa kipindi fulani.

Kuhusu Pazia, inafaa kusema kwamba hakuna chochote chenye kufichika na uoni wa Allaah. Sisi tumefichikamana Naye duniani ilihali makafiri wamefichikamana Naye duniani na Aakhirah. Hata hivyo imesihi kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah halali na wala haimstahikii Yeye kulala. Anaishusha mizani na kuinyanyua. Kwake kunapandishwa matendo ya usiku kabla ya mchana na matendo ya mchana kabla ya usiku. Pazia Yake ni Nuru; lau ataifunua, basi mwanga wa uso Wake ungeliunguza kila anachoona katika uumbaji Wake.”[1]

Tunayaamini hayo, hatuhoji na tunasimamia hapo.

[1] Muslim (179).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/235)
  • Imechapishwa: 04/11/2020