Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutoka kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mimi nitakutangulieni kwenye hodhi. Wanaume katika Ummah wangu watanyanyuliwa kwangu na pindi ninapoenda kuwachukua, watawekwa mbali na mimi ambapo nitasema: “Ee Mola! Wafuasi wangu!” Kusemwe: “Hakika wewe hujui waliyozusha baada yako.”[1]

MAELEZO

Katika tamko jingine imekuja:

”Hawakuacha kuwa ni wenye kuritadi [kwenye visigino vyao] tangu ulipoachana nao.”[2]

Kwa ajili hii watazuiwa kutokamana na hodhi. Kwa sababu wameritadi. Wale walioritadi katika zama za Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) watazuiwa kutokamana na hodhi. Kuhusu ambaye alikufa juu ya imani yake ataifikia hodhi.

[1] al-Bukhaariy (7049) na Muslim (2297).

[2] Tazama ”Sharh-un-Nawawiy ´alaa Swahiyh Muslim” (03/135) na ”Fath-ul-Baariy” (06/226) ya Ibn Hajar.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 40-41
  • Imechapishwa: 05/11/2020