Husema mara nyingi kuwaambia ndugu zangu barua ya ‘Abdul-‘Aziyz bin Baaz inakumbusha barua za al-Awzaa’iy. Baadhi ya barua za al-Awzaa´iy zimetajwa katika utangulizi wa “al-Jarh wat-Ta’diyl” wakati alipokuwa akimnasihi mtawala na akiwaombea wengine. Kadhalika ndivyo Shaykh ‘Abdul-‘Aziyz. Amemuandikia mtoto wa mfalme, hakimu, mkuu wa idara ya hati ya kusafiri na akiombea [watu wengine kwa] mamlaka. Allaah amjaze kheri.

Ahl-us-Sunnah! Tambueni ya kwamba wale wanaomsema vibaya ni kwa sababu ni Sunniy, neno lake linasikika na kwa sababu wao wenyewe hawana mwanachuoni yeyote kama yeye. Wameshughulishwa na Hizbiyyah. La sivyo nimesoma na watu wengi katika chuo kikuu ambao wamepata shahada yao na walikuwa na akili sana. Baada ya muda wakageuka katika u-Hizbiyyah. Hizbiyyuun hawana mwanachuoni yeyote kama Shaykh Ibn Baaz. Ndio maana hawamsemi vibaya katika Ahl-us-Sunnah kama Shaykh Ibn Baaz.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 30-31
  • Imechapishwa: 26/08/2020