Lau punda ingeliweza kuzungumza basi ingelitoa maoni yake. Kuna tofauti kati ya bunge na mashauriano (Shuuraa´).

Upande wa kwanza mashauriano yanafanywa na wanachuoni wenye busara na watawala.

Upande wa pili, bunge inakuwa na waombaji ambao hamu yao kubwa ni kupata uongozi, wamiliki wa migahawa bali mpaka wanawake ambao na wao [wanataka] kufikisha mapendekezo yao na wanayofikiri. Je, huu ni Uislamu?

Kama ni kweli kuwa Shaykh Ibn Baaz na Shaykh Ibn ‘Uthaymiyn wanajuzisha hilo, hivyo mimi nawapinga na kuwakataza. Hata hivyo, kosa lolote linafutwa na wema wao. Kadhalika wanapewa udhuru kwa kuwa wametiwa mchanga wa machoni. Himdi zote ni Zake Allaah kwa vile Ahl-us-Sunnah hawafuati kichwa mchunga. Sisi sio kama mshairi alivosema:

Kama mfano wa ng’ombe kipofu anayeongozwa na mchungaji kipofu

kwenye njia iliyopinda

Tunajisalimisha kwa Allaah na si kwa watu:

وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيْهِ يَقُولُ يَا لَيْتَنِي اتَّخَذْتُ مَعَ الرَّسُولِ سَبِيلًا يَا وَيْلَتَىٰ لَيْتَنِي لَمْ أَتَّخِذْ فُلَانًا خَلِيلًا لَّقَدْ أَضَلَّنِي عَنِ الذِّكْرِ بَعْدَ إِذْ جَاءَنِي ۗ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِلْإِنسَانِ خَذُولًا

“Na siku dhalimu atakapotafuna mikono yake akisema: “Laiti ningechukua pamoja na Mtume njia. Ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki mwandani wangu. Kwani hakika amenipoteza mbali na Ukumbusho baada ya kunijia.” – na daima shaytwaan kwa mtu ni mwenye kumtosa.” (25:27-29)

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Naswaaih wa Fadhwaaih, uk. 137
  • Imechapishwa: 26/08/2020