Swali: Katika Tarawiyh tunawaona baadhi wanasimama baada imamu kutoa Tasliym kumaliza Witr na Witr yao inakuwa mwisho wa usiku. Je, kitendo hichi ndio bora au bora ni mtu atosheke na Witr pamoja na imamu?

Jibu: Haya ni maoni ya baadhi ya wanazuoni. Bora ni yeye atosheke na Witr pamoja na imamu na [akitaka] aswali mwishoni mwa usiku. Kufanya ndio kuko mbali zaidi na kujionyesha.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (22)
  • Imechapishwa: 31/10/2021