Amesahau kusoma Suurah nyingine baada ya al-Faatihah

Swali: Niliswali Dhuhr peke yangu na katika Rak´ah ya pili sikusoma Suurah nyingine baada ya “al-Faatihah” hali ya kusahau. Nikasujudu sijda ya kusahau pindi nilipokumbuka punde kidogo kabla ya kuleta Tasliym. Je, kuna neno kwangu kwa kufanya hivo?

Jibu: Huna neno. Wala haikulazimu kusujudu sijda ya kusahau. Kwa sababu kusoma Suurah baada ya al-Faatihah au kile kitachokuwia chepesi katika Aayah sio lazima. Jambo la lazima ni kusoma al-Faatihah. Aidha imependekezwa kusoma Suurah nyingine baada yake katika Rak´ah ya kwanza na ya pili ya kila swalah. Ukisujudu sijda ya kusahau ni sawa na swalah yako ni sahihi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/272)
  • Imechapishwa: 31/10/2021